Your cart is empty, and it looks like you haven’t added anything yet.
Mshahara umeingia. Kabla haujaisha kwenye matumizi mengine, amua leo ni awamu gani ya nyumba yako utaigharamia mwezi huu. Watanzania wengi hujenga kwa awamu, na hiyo ni sawa kabisa, ilimradi kila awamu ina mpango, orodha ya vifaa na bajeti.
| Awamu | Kazi kuu | Vifaa vikuu |
|---|---|---|
| 1. Msingi | Kuchimba, zege la msingi, kuta za msingi | Saruji, mchanga, kokoto, nondo na waya wa kufungia, tofali |
| 2. Boma hadi lenta | Kujenga kuta, kumwaga lenta | Tofali, saruji, mchanga, nondo |
| 3. Paa | Mbao au chuma, mabati, mifereji ya maji | Mbao, mabati, misumari ya paa, gutters |
| 4. Umeme na maji | Kupitisha nyaya na mabomba | Nyaya na vifaa vya umeme, mabomba na viungio |
| 5. Finishing | Plasta, sakafu, bafu, milango, rangi | Saruji, vifaa vya bafu na vyoo, marumaru, kufuli, rangi |
Muulize fundi wako akupe idadi ya vifaa (au angalia BOQ ya mhandisi). Kisha jaza bei ya leo kutoka kwenye ukurasa wa kila bidhaa.
| Kifaa | Idadi (kutoka kwa fundi) | Bei ya kipimo kimoja (leo) | Jumla |
|---|---|---|---|
| Saruji (mfuko kilo 50) | |||
| Nondo | |||
| Tofali | |||
| Mchanga na kokoto | |||
| Usafiri | |||
| Ufundi (labour) | |||
| Akiba ya dharura (10–15%) |
Akiba ya dharura inakulinda bei zikipanda au kazi ikihitaji vifaa vya ziada. Mwaka 2026 bei za saruji na nondo zimepanda, kwa hiyo usiiruke.
Kwenye Ujenzi Direct, ada ya usafiri inaonyeshwa kabla ya kulipa. Inategemea uzito, ujazo na umbali. Tunaleta ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Jumatatu hadi Jumamosi. Unaweza pia kuchukua mwenyewe dukani kwa muuzaji popote Dar es Salaam pale inapopatikana.
Lipa kwa simu au AzamPay, au chagua kulipa ukipokea (cash on delivery) pale inapoonyeshwa. Hatutoi mkopo; kila oda hulipwa kabla ya kusafirishwa au wakati wa kupokea.
Hakuna bei moja: inategemea ukubwa, ramani, eneo, ubora wa vifaa na bei za siku hiyo. Tumia jedwali hili kwa kila awamu, kwa idadi kutoka kwa fundi au mhandisi wako.
Kwa ramani iliyoidhinishwa na makadirio ya vifaa (BOQ). Kisha anza na msingi, awamu inayohitaji usahihi zaidi.
Ndiyo. Unaweza kuagiza kwa kila awamu, na kwa saruji kuanzia mifuko 5.
Anza awamu yako leo: angalia aina zote za vifaa kwenye Ujenzi Direct.
You need to Sign in to view this feature
This address will be removed from this list